Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 94

An-Nahl 16:94

النحل

وَلَا تَتَّخِذُوٓا۟ أَيْمَـٰنَكُمْ دَخَلًۢا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌۢ بَعْدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا۟ ٱلسُّوٓءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ وَلَكُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Maana

Wala msifanye viapo vyenu kuwa njia ya kudanganyana baina yenu, mguu ukajateleza baada ya kuwa thabiti, na mkaonja mabaya kwa sababu ya kule kuzuilia kwenu njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msifanye viapo vyenu ni njia ya kudanganyana baina yenu.Usije mguu ukateleza badala ya kuthibiti, na mkaonja maovu kwa sababu ya kule kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa. [94]

[94] Wala msishike njia ya khiana, mkafanya viapo ndio njia ya udanganyifu na khadaa. Kwa hivyo nyayo zenu zitateleza mlikosee lengo lilio sawa, na kwa hivyo ikapelekea mkaiwacha Njia ya Mwenyezi Mungu ya kutimiza ahadi, na mkawa ni mfano muovu wa khiana, na watu wakaja waona kuwa Waislamu ni watu wabaya, na wakautupilia mbali Uislamu wenyewe. Na uovu ukateremka duniani kwa sababu yenu kwa kuto kuaminini kwa vile mnavyo kwenda kinyume na njia ya haki, nanyi ikakuteremkieni adhabu kali yenye kutia machungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala msifanye, kati ya viapo mnavyoviapa, udanganyifu kwa wale mliowaapia, mkaja kuangamia baada ya kuwa kwenye amani. Ni kama yule ambaye nyayo zake ziliteleza baada ya kuwa zimekita. Na mtaonja adhabu ya kuwaudhi ulimwenguni kwa vile mlisababisha kuwakataza wengine na Dini hii kwa ukiukaji ahadi waliouona kutoka kwenu, na huko Akhera mtapata adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net