An-Nahl 16:95
النحلوَلَا تَشْتَرُوا۟ بِعَهْدِ ٱللَّهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ إِنَّمَا عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Wala msinunue kwa agano la Mwenyezi Mungu thamani ndogo. Hakika kilicho kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Hakika kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua. [95]
[95] Wala msibadilishe ahadi ya kweli kweli kwa kutaka pato la dunia, na hilo ni duni na lingali onekana kubwa. Maana yaliopo kwa Mwenyezi Mungu, malipo ya wanao hifadhi ahadi zao duniani, na malipo ya Akhera ya milele, ni bora kwenu kuliko yote yanayo kudanganyeni kwa kuvunja ahadi. Basi zingatieni na mfahamu, ikiwa nyinyi ni watu wa ilimu na utambuzi baina ya jema na lisio kuwa jema. Wala msitende ila lilio na maslaha kwenu duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wala msivunje ahadi ya Allah Mtukufu kwa kuchukua badala yake kitu kidogo cha starehe ya duniani. Hakika malipo mema yaliyoko kwa Allah Mtukufu ya utekelezaji ahadi ni bora kwenu kuliko thamani hii ndogo. Basi iwapo nyinyi ni watu mnaojua, zingatieni tafauti iliyopo baina ya mazuri mawili haya: ya ulimwenguni na ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net