Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 96

An-Nahl 16:96

النحل

مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓا۟ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Mlivyo navyo vitakwisha, na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyo bakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa walio subiri ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda. [96]

[96] Kwani neema mlizo nazo zina mwisho hata zingeli kaa muda mrefu. Na neema zilioko kwa Mwenyezi Mungu Akhera ni za milele wala hazishi. Na Sisi tutawalipa wenye kuvumilia mashaka ya taabu kwa ajili ya tuliyo waahidi, nayo ni kupata bora ya malipo marudufu kwa vitendo vyao, waneemeke kwayo daima milele Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo mliyonayo, miongoni mwa taka za kilimwengu, yataondoka na yale yaliyoko kwa Allah Mtukufu, ya riziki na thawabu, hayataondoka. Na wale waliohimili kubeba mazito ya Sheria waliyotakiwa wayabebe, miongoni mwayo ikiwa ni utekelezaji ahadi, tutawalipa malipo mazuri zaidi ya matendo yao mema: tutawapa zaidi kwa matendo yao madogo kama tutakavyowapa zaidi kwa matendo yao makubwa kwa ukarimu wetu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net