An-Nahl 16:97
النحلمَنْ عَمِلَ صَـٰلِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, hakika tutamhuisha uhai mwema, na hakika tutawapa ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda. [97]
[97] Hakika mwenye kutenda mema duniani, sawa sawa akiwa mwanamume au mwanamke, akajiingiza katika huo wema kwa nguvu za imani, kwa kila linalo wajibika kwa kuliamini, basi Sisi hatuna budi kumfanya aishi maisha mazuri yasiyo kuwa na machungu, yenye ndani yake ukinaifu na kuridhika na kuvumilia masaibu ya dunia, na shukrani kwa neema anazo zipata kwa Mwenyezi Mungu. Na Akhera hapana budi ya kuwa tutawalipa watu wa namna hii bora ya malipo kwa kuzidi marudufu kwa vitendo vyao vya duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenye kufanya tendo zuri, akiwa ni mwanamume au ni mwanamke, na huku ni mwenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, basi tutampa maisha mema yenye utulivu duniani hata kama ni mchache wa mali, na tutawalipa huko Akhera thawabu zao kwa uzuri zaidi ya walivyofanya duniani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net