An-Nahl 16:98
النحلفَإِذَا قَرَأْتَ ٱلْقُرْءَانَ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ ٱلرَّجِيمِ
Na unaposoma Qur-ani, mwombe Mwenyezi Mungu akulinde kutokana na Shetani aliyelaaniwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni. [98]
[98] Kinacho linda nafsi isighurike na pumbao ni Qur'ani. Ewe Muumini! Ukitaka kuishi maisha ya mbali na kuchezewa na Shetani, na upate wema wa kote kuwili, duniani na Akhera, basi Mimi nakuongoza kwenye jambo litakalo kusaidia kwa hayo. Jambo lenyewe ni kuisoma Qur'ani. Na unapo taka kusoma Qur'ani, anzia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi akuepushe na wasiwasi wa Shetani, aliye fukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na anaona uzuri kuwaghuri watu awaingize katika kumuasi Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi ukitaka, ewe Muumini, kusoma chochote katika Qur’ani, basi jilinde kwa Allah Mtukufu na Shari la Shetani aliyefukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu kwa kusema, «A‛ûdhu bi- Llãhi min ash-Shaytṭãn ar-Rajîm» (Najilinda kwa Allah Mtukufu na Shetani Aliyefukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net