An-Nahl 16:99
النحلإِنَّهُۥ لَيْسَ لَهُۥ سُلْطَـٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ
Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi. [99]
[99] Ukifanya haya kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, basi atakulinda na Shetani, na atakuondolea wasiwasi. Kwani Shetani hana athari kwa walio jaa Imani ya Mwenyezi Mungu, na wakamtaka msaada na kumtegemea Yeye peke yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, Shetani hana uwezo wa kuwasaliti wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wanaomtegemea Mola wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net