Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 100

An-Nahl 16:100

النحل

إِنَّمَا سُلْطَـٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشْرِكُونَ

Maana

Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, na wale wanaofanya ushirika naye.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika madaraka yake ni juu ya wanao mfanya rafiki yao, na wale wanao fanya ushirika naye. [100]

[100] Bali taathira yake Shetani na khatari yake ni juu ya wale ambao nyoyo zao hazina mfungamano wala mapenzi na Mwenyezi Mungu. Basi hao hawana la kuwalinda na athari za Shetani. Watamfuata huyo kama rafiki anavyo mfuata rafiki yake, mpaka watumbukie katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika kumuabudu pamoja na miungu mingine isiyo weza kuleta madhara wala manufaa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Uwezo wake wa kusaliti ni juu ya wale waliomfanya yeye ni msaidizi wao na wakamtii na wale ambao wao, kwa sababu ya kumtii yeye, wanamshirikisha Allah Mtukufu Aliyetukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net