Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 101

An-Nahl 16:101

النحل

وَإِذَا بَدَّلْنَآ ءَايَةً مَّكَانَ ءَايَةٍ ۙ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مُفْتَرٍۭ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Na tunapobadilisha Ishara pahala pa Ishara, na Mwenyezi Mungu anayajua anayoyateremsha, wanasema: "Wewe si chochote ila ni mzushi tu", lakini wengi wao hawajui tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tunapo badilisha Ishara pahala pa Ishara nyengine, na MwenyeziMungu anajua anayo teremsha, wao husema: Wewe ni mzushi. Bali wengi wao hawajui kitu. [101]

[101] Na tukikuletea muujiza badala ya muujiza ulio sawa na tulio waletea Manabii walio tangulia, na tukakuletea wewe hii Qur'ani kuwa ni muujiza wenyewe, wanakusingizia kuwa umeizua tu hii, na kwamba unamzulia Mwenyezi Mungu uwongo! Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mjuzi kwa ujuzi usio pikuliwa kuijua miujiza anayo wateremshia Manabii wake. Lakini wengi wao watu hawa si watu wa ilimu wa kujua lilio kweli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tunapoibadilisha aya kwa aya nyingine, na Allah Mtukufu Mwenye kuumba Anayajua zaidi maslahi ya viumbe Wake kwa hukumu Anazoziteremsha katika nyakati mbalimbali, makafiri wanasema, «Hakika yako wewe, Ewe Muhammad, ni mrongo mwenye kumzulia Allah Mtukufu Asiyoyasema.» Na Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amni zimshukie), si kama wanavyodai kwamba ni muongo. Lakini wengi wao hawana ujuzi juu ya Mola wao wala kuhusu Sheria Yake na hukumu Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net