An-Nahl 16:102
النحلقُلْ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلْحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ
Sema: Ameiteremsha Roho Mtakatifu kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa haki, ili iwaimarishe wale walioamini, na kuwa ni uongofu, na bishara kwa Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu. [102]
[102] Ewe Nabii! Waambie kuwabainishia muujiza wako: Hakika hii Qur'ani kaniteremshia mimi Jibril, Roho safi, kutokana kwa Mola wangu Mlezi, kwa kufuatana na kukusanya Haki, ili kwayo azitie imara nyoyo za Waumini, na ili iwe ni Uwongofu kwa watu wote waongokewe, na iwape bishara njema ya neema Waislamu wote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, Qurani haikuzuliwa na mimi, bali aliyeiteremsha ni Jibrili kutoka kwa Mola wako kwa ukweli na uadilifu ili kuwafanya Waumini wawe imara, kuwaongoza wao kutoka kwenye upotevu, na kuwapa bishara njema wale waliojisalimisha na kunyenyekea kwa Allah Mtukufu, Bwana wa viumbe wote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net