An-Nahl 16:103
النحلوَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُۥ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ ٱلَّذِى يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِىٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِىٌّ مُّبِينٌ
Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: "Hakika yuko mtu anayemfundisha." Lugha ya huyo wanayemuelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu iliyo bainifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha.Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu mbayana. [103]
[103] Hakika Sisi tunajua wayasemayo makafiri wa Makka, nayo: Hamfundishi Muhammad hii Qur'ani ila mtu tunaye mjua, naye ni kijana wa Kirumi. Wala hamteremshii Malaika kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama asemavyo! Na kauli yao hii ni ya uwongo. Kwani huyo kijana wanaye sema kuwa anakufundisha wewe ni mgeni, hajui Kiarabu vizuri. Na Qur'ani ni lugha ya Kiarabu kilicho wazi cha ufasihi, hata imekuwa nyinyi wabishi mmeshindwa kuleta mfano wake. Basi hizo tuhuma zenu zina maana gani?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tunajua kuwa washirikina wanasema kwamba Nabii anapokea Qur’ani kutoka kwa kiumbe miongoni mwa wanadamu. Wamesema urongo! Kwani lugha ya yule waliomsingizia kuwa amemfundisha Nabii, (rehema na amani zimshukie), si ya Kiarabu na hii Qur’ani ni kwa lugha ya Kiarabu, imefikia upeo wa hali ya juu wa ufafanuzi na ubainifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net