An-Nahl 16:44
النحلبِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَٱلزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ
Kwa Ishara wazi na Vitabu. Na tumekuteremshia ukumbusho huu ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, ili wapate kutafakari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri. [44]
[44] Na hao Mitume tuliwaunga mkono kwa miujiza na dalili zilizo wazi za kuthibitisha ukweli wao. Na tuliwateremshia Vitabu vya kuwabainishia sharia zao zenye maslaha yao. Na wewe, ewe Nabii, tumekuteremshia Qur'ani uwabainishie watu Itikadi na Hikima ziliomo ndani yake, na uwatake waizingatie, kwa kutaraji kuwa watazingatia, na watawaidhika, na mambo yao yanyooke.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwatuma Mitume waliotangulia wakiwa na dalili za waziwazi na vitabu vya mbinguni. Na tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani upate kuwafunulia watu maana yake na hukumu zake zilizofichika, na ili wapate kuizingatia na waongoke kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net