An-Nahl 16:43
النحلوَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۚ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Nasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume tuliowapa ufunuo (wahyi). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi(Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui. [43]
[43] Na kabla ya kukutuma wewe, ewe Nabii, kwa umma wako, hatukuwatuma kwa kaumu zilizo tangulia ila watu wanaume tulio wafunulia kwa Wahyi yale tunayo yataka wawafikishie. Wala hatukuwatuma Malaika kama watakavyo makafiri wa kaumu yako. Basi, enyi makafiri, waulizeni wenye kuvijua Vitabu vya mbinguni, kama nyinyi hamyajui hayo. Watajua kuwa Mitume wote wa Mwenyezi Mungu hawakuwa ila wanaadamu, wala si Malaika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukuwatuma kwa waliotangulia kabla yako, ewe Mtume, isipokuwa Mitume miongoni mwa wanaume, sio Malaika, tunaowaletea wahyi. Na iwapo nyinyi, enyi washirikina wa Kikureshi, hamliamini hilo, basi waulizeni waliopewa vitabu vilivyopita, watawapa habari kwamba Manabii walikuwa ni binadamu, mkiwa hamjui kwamba wao ni binadamu. Aya hii inakusanya kila suala kati ya masuala ya Dini, iwapo mtu hana ujuzi nalo amuulize anayelijua miongoni mwa wanavyuoni waliozama katika elimu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net