An-Nahl 16:42
النحلٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ
Wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale wanao subiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi. [42]
[42] Na hao Wahajiri (Walio hama) ndio walio vumilia adhabu walio ipata kwa sababu ya Itikadi yao, na wakamwachia hali yao Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya kumbali mwenginewe. Kwa ajili ya hayo tumewapa bora ya malipo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa wenye kuhama katika njia ya Allah Mtukufu ndio waliovumilia juu ya amri ya Allah Mtukufu na makatazo Yake na juu ya makadirio Yake yenye uchungu, na kwa Mola wao Peke Yake wanategemea, ndipo wakastahiki cheo hiki kikubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net