An-Nahl 16:41
النحلوَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ فِى ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ
Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, bila ya shaka tutawaweka katika maskani mazuri katika dunia; na hakika ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; lau wangekuwa wanajua!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa,bila ya shaka tutawaweka duniani kwa wema; na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti kuwa wanajua! [41]
[41] Na Waumini walio yaacha majumba yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na usafi wa imani yao, baada ya kudhulumiwa na washirikina, tutawalipa duniani, kwa ikhlasi yao na kustahamili kwao adhabu, maisha mema yasiyo patikana ila kwa jihadi. Na Siku ya Kiyama ujira wao utakuwa mkubwa zaidi, na neema zao za Peponi ni kubwa zaidi. Lau kuwa wapinzani wao wangeli jua hayo wasingeli wadhulumu na wakazidhulumu nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale walioacha makao yao kwa ajili ya Allah Mtukufu na wakahama baada ya matukio ya kudhulumiwa, tutawakalisha duniani makao mema. Na malipo ya Akhera ni makubwa zaidi, kwani malipo yao huko ni Pepo. Lau wale waliosalia nyuma wakaacha kuhama wangejua, ujuzi wa uhakika, yale yaliyoko kwa Allah Mtukufu ya malipo na thawabu kwa wale wanaohama katika njia Yake, asingesalia nyuma yoyote katika wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net