An-Nahl 16:40
النحلإِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَىْءٍ إِذَآ أَرَدْنَـٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Hakika, kauli yetu kwa kitu tunapokitaka kiwe, ni kukiambia tu: "Kuwa!" Basi kinakuwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kauli yetu kwa kitu tunacho kitaka kiwe, ni kukiambia: Kuwa!Basi kinakuwa. [40]
[40] Na kuwafufua watu Siku ya Kiyama si jambo zito kwetu, hata hao makafiri wakayaona hayawi. Kwani Sisi tutakapo kitu kiwe hatuna haja ya lolote ila ni kusema tu: Kuwa! Na kinakuwa kama tutakavyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika jambo la kufufua ni lepesi kwetu. Kwani sisi tutakapo kitu, tunakiambia «Kuwa» ukitahamaki kimeshakuwa na kimeshapatikana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net