An-Nahl 16:39
النحللِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِى يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ كَـٰذِبِينَ
Ili awabainishie yale waliyohitilafiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili kuwabainishia yale waliyo khitalifiana, na ili wajue waliokufuru kwamba wao walikuwa ni waongo. [39]
[39] Hakika katika uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni kuwa atawafufua wote baada ya kufa kwao ili ipate wadhihirikia hakika ya mambo waliyo khitalifiana. Waumini wapate kujua kuwa wao wako katika Haki, na makafiri wajue kwamba wao walikuwa makosani kwa kumfanyia Mwenyezi Mungu washirika katika Ungu, na pia ni waongo kwa kuapa kwao kwamba Mwenyezi Mungu hamfufui aliye kufa, na ili yote makundi mawili yapate malipo yao kwa kujua na kwa sababu zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Atawafufua waja wote, ili awafunulie ukweli wa Ufufuzi ambao wametafautiana juu yake, na ili makafiri wenye kuukanusha wapate kujua kwamba wao wako kwenye ubatilifu na kwamba wao ni warongo pindi walipoapa kwamba hakuna kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net