An-Nahl 16:38
النحلوَأَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُ ۚ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatamfufua aliyekufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini wengi wa watu hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba MwenyeziMungu hatomfufua aliye kufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini watu wengi hawajui. [38]
[38] Na washirikina juu ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu wameongezea kuikanusha Siku ya Kiyama. Wameapa, ukomo wa nguvu zao za kuapa, na wakakazania kwamba Mwenyezi Mungu hamfufui aliye kufa! Nao ni waongo katika viapo vyao, na Mwenyezi Mungu atawafufua wote! Kwani Yeye amejichukulia ahadi mwenyewe, na Mwenyezi Mungu kabisa hatokwenda kinyume na ahadi yake. Lakini watu wengi miongoni mwa makafiri hawaijui hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuumba huu ulimwengu, na kwamba Yeye hakuumba kwa mchezo tu, wala wao hawajui hisabu yake na malipo yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa washirikina waliapa kwa Allah Mtukufu viapo vizito kwamba Allah Mtukufu Hatamfufua aliyekufa baada na kumalizika na kutawanyika. Kwani, Atawafufua Allah Mtukufu kwa lazima, hiyo ni ahadi ya kweli Aliyojilazimisha nayo, lakini wengi wa watu hawaujui uwezo wa Allah Mtukufu wa kufufua, ndio maana wanaukanusha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net