An-Nahl 16:37
النحلإِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَىٰهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى مَن يُضِلُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ
Hata ukiwa na pupa juu ya kuongoka kwao, basi hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anayeshikilia kupotea. Wala hawatapata yeyote wa kuwanusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anaye shikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru. [37]
[37] Ewe Nabii! Ikiwa una hamu mno ya kuwaongoa washirikina katika watu wako, kwa kutumia ukomo wa juhudi yako, basi usiihiliki nafsi yako kwa huzuni ikiwa hayo uyatakayo hayawi. Kwani hao wamekwisha milikiwa na matamanio. Na Mwenyezi Mungu hawalazimishi kuongoka walio khiari upotovu na wakaushikilia, kwani Yeye huwaacha wajichagulie wenyewe, nao watapata malipo yao, nayo ni adhabu kubwa. Na wala hawatapata Siku ya Kiyama wa kuwanusuru na kuwalinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Utakapofanya bidii yako ya mwisho, ewe Mtume, kuwaongoa hawa washirikina, basi jua kwamba Allah Mtukufu Hamuongozi Anayepotosha, na hawana wao yoyote asiyekuwa Allah Mtukufu atakayewaokoa na kuwazuilia adhabu Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net