Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Sura ya 16

An-Nahl

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 41

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ فِى ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ 41

{41} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu fadhila za waumini wanaojaribiwa, "wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Yaani, katika njia yake na kutafuta radhi zake, "baada ya kudhulumiwa" kwa kuudhiwa, kujaribiwa na kaumu yao ili wawarudishe katika ukafiri na ushirikina. Kwa hivyo wakaacha miji yao na marafiki zao, na wakayahama hayo kwa ajili ya kumtii Mwingi wa rehema. Kwa hivyo akataja kwamba wana thawabu mbili: thawabu ya haraka katika dunia kama vile riziki pana, na maisha mazuri ambayo waliyaona kwa macho baada ya kuhama na kuwashinda maadui zao na wakaiteka miji na wakapata ngawira nyingi kutoka kwao. Kwa hivyo wakazifanya kuwa mali zao, na Mwenyezi Mungu akawapa mazuri katika dunia, "na ujira wa Akhera" aliyowaahidi juu ya ulimi wa Mtume wake ni bora na "makubwa zaidi" kuliko malipo ya dunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofuzu. Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. Watadumu humo milele. Hakika Mwenyezi Mungu kwake anayo malipo makubwa." Na kauli yake, "lau wangekuwa wanajua" malipo na thawabu zilizopo kwa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuamini na akahama katika njia yake, basi hakuna yeyote aliyeangalia kando na hayo!