An-Nahl 16:45
النحلأَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخْسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ ٱلْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ
Je wana amani wale wanaopanga njama mbaya kwamba Mwenyezi Mungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafikia adhabu kutoka wasipohisi?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Wameaminisha wanao fanya vitimbi vya uovu kwamba MwenyeziMungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafika adhabu kutoka wasipopajua? [45]
[45] Yafaa vipi basi baada ya yote haya kuwa hao washirikina wakaendelea katika inda yao, na wakampangia vitimbi Mtume? Je, kwani wamedanganyika na upole wa Mwenyezi Mungu kwao, hata wakaitakidi kuwa wameaminika na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na ardhi haitowameza kama ilivyo mfanyia Qaaruun? Au kuwa adhabu haitowajia kwa ghafla katika kimbunga kama ilivyo wapata kina Thamud nao hawajui inatoka wapi?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, wanajiaminisha wale makafiri wanaopanga vitimbi kwamba Allah Mtukufu Hatawadidimiza ndani ya ardhi kama Alivyomfanya Qãrûn au kwamba adhabu haitawafikia kutoka mahali wasipopadhania na wasipopatarajia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net