An-Nahl
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَٱلزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ 44
{44} Na walio bora zaidi katika wenye ukumbusho ni watu wa Qur-ani hii tukufu. Kwa maana, wao ndio watu wa ukumbusho kiuhakika, noa ndio wanaolifailia zaidi jina hili kuliko watu wengineo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho;" yaani, Qur-ani hii ambayo ndani yake kuna ukumbusho wa wale wanayoyahitaji ya mambo ya dini yao na dunia yao, ya dhahiri na ya ndani. "Ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao" Na hili linajumuisha kubainisha matamshi yake na maana zake. "ili wapate kutafakari" kitabu hiki, na kutoa katika hazina zake na elimu zake kulingana na utayari wao na kukielekea kwake.