Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 36

Ar-Ra'd 13:36

الرعد

وَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَفْرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ ۖ وَمِنَ ٱلْأَحْزَابِ مَن يُنكِرُ بَعْضَهُۥ ۚ قُلْ إِنَّمَآ أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشْرِكَ بِهِۦٓ ۚ إِلَيْهِ أَدْعُوا۟ وَإِلَيْهِ مَـَٔابِ

Maana

Na wale tuliowapa Kitabu wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake. Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe. Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulio wapa Kitabu wanafurahia uliyo teremshiwa. Na katika makundi mengine wapo wanao yakataa baadhi ya haya. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, na wala nisimshirikishe. Kuendea kwake Yeye ndiyo ninaita, na kwake Yeye ndio marejeo yangu. [36]

[36] Na wale ambao walio pewa ujuzi wa Vitabu vilivyo teremshwa ni waajibu wao wakifurahie Kitabu hichi ulicho teremshiwa wewe. Kwani hichi ni maendeleo ya ule ule ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Na wanayo ifanya dini kuwa ni sababu ya kufanya makundi mbali mbali wanayakataa baadhi ya uliyo teremshiwa kwa uadui na chuki tu. Basi ewe Nabii! Waambie: Hakika mimi sikuamrishwa ila nimuabudu Mwenyezi Mungu, na nisimshirikishe katika ibada yake na kitu chochote. Na kwendea kumuabudu Yeye peke yake ndio ninalingania, ninaita, na kwake Yeye peke yake ndio marejeo yangu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao tuliwapa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na manaswara, yoyote kati yao mwenye kukuamini, kama ‛Abdullãh bin Salãm na Najãshî, wanaifurahia Qur’ani uliyoteremshiwa kwa kuwa inaenda sambamba na kile walichonacho. Na miongoni mwa wale wanaojiweka pamoja kukupinga, kama Sayyid na ‛Ãqib: maaskofu wawili wa Najrãn, na Ka‛b bin al- Ashraf, wanaokanusha baadhi ya yale uliyoteremshiwa. Waambie, «Allah Mtukufu Ameniamrisha nimuabudu Yeye Peke Yake na nisimshirikishe chochote. Nawaita watu wamuabudu, na Kwake Peke Yake ndio marejeo yangu na marudio».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net