Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 37

Ar-Ra'd 13:37

الرعد

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَـٰهُ حُكْمًا عَرَبِيًّا ۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعْتَ أَهْوَآءَهُم بَعْدَ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا وَاقٍ

Maana

Na ndivyo hivyo tumeiteremsha (Qur-ani hii kuwa ni) hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya elimu hii iliyokujia, hutakuwa na rafiki yeyote wala mlinzi kando na Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ndio kama hivi tumeiteremsha Qur'ani kuwa ni hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya kukujia ilimu hii, hutakuwa na rafiki wala mlinzi mbele ya Mwenyezi Mungu. [37]

[37] Na kama vilivyo teremka Vitabu vya mbinguni, tumekuteremshia wewe hii Qur'ani ili iwe ni hakimu baina ya watu kwa yaliyo baina yao, na iwe ni hakimu wa Vitabu vilivyo tangulia kuwa ni vya kweli. Na hii Qur'ani tumeiteremsha kwa lugha ya Kiarabu. Wala usitake kuwafurahisha washirikina au Ahli Lkitab (watu wa Biblia), baada ya ufunuo na ilimu iliyo kufikia. Na ukitaka kuwaridhi basi hutakuwa na wa kukusaidia au kukulinda mbele ya Mwenyezi Mungu. Hapa anaambiwa Nabii, khasa wanasemezwa Waumini wote. Na mahadharisho ya Waumini ni kweli kweli hivyo; na kwa Nabii ni kwa ajili ya kubainisha kuwa juu ya kuwa yeye ni mteuliwa, na mtukufu wa daraja, bado anafaa kuhadharishwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyowateremshia Mitume Vitabu kwa lugha zao, tulikuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani kwa lugha ya Kiarabu, ili uitumie katika kuhukumu. Na lau ungefuata mapendeleo ya washirikina katika kumuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu, baada ya haki iliyokujia kutoka kwa Allah Mtukufu, usingekuwa na msaidizi yoyote mwenye kukuhami na kuzuia adhabu ya Allah Mtukufu isikufikie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net