Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 38

Ar-Ra'd 13:38

الرعد

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَٰجًا وَذُرِّيَّةً ۚ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِىَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۗ لِكُلِّ أَجَلٍ كِتَابٌ

Maana

Na hakika Sisi tulikwishawatuma Mitume kabla yako, na tukawafanya wawe na wake na dhuria. Na haikuwa kwa Mtume yeyote kuleta ishara isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake iliyoandikwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya. Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipo kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake. [38]

[38] Na ikiwa washirikina wanachochea watu wastaajabu kuwa wewe una wake na dhuriya, yaani wazao, na wanataka ulete muujiza mwengine usio kuwa Qur'ani, basi tulileta kabla yako Mitume wenye wake na wana vile vile. Kwani Mtume ni mwanaadamu, na ana sifa za kibinaadamu. Lakini yeye ni mbora kuliko wote. Wala Nabii hawezi kuleta muujiza kama apendavyo yeye au wapendavyo watu wake! Bali aletaye muujiza ni Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye anaye toa idhini. Kila kizazi katika vizazi kina amri yao aliyo waandikia Mwenyezi Mungu ya kuwasilihi. Na kila kizazi kina muujiza wake unao wanasibu. (Nabii Isa a.s. anasimuliwa katika Injili ya Yohana 5.30 kuwa alisema: Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka waliposema, «Una nini, ewe Mtume, unaoa wanawake?» Hakika tulituma kabla yako Mitume kati ya wanadamu na kuwafanya wawe na wake na watoto. Na pia kumbuka waliposema, «Lau angekuwa ni Mtume angalituletea miujiza tuliyoitaka.» Haiko kwenye uwezo wa Mtume yoyote, kuleta miujiza ambayo watu wake waliitaka isipokuwa kwa idhini ya Allah Mtukufu. Kila jambo alilolihukumu Allah Mtukufu lina maandishi na wakati, Allah Mtukufu Ameliandika hapo Kwake, halitangulii wala halichelewi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net