Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 39

Ar-Ra'd 13:39

الرعد

يَمْحُوا۟ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُۥٓ أُمُّ ٱلْكِتَـٰبِ

Maana

Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na kiko kwake Kitabu asili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake. [39]

[39] Mwenyezi Mungu hufuta sharia na miujiza, na akaleta badala yake atakayo na akaithibitisha. Na kwake Yeye ipo asili ya Sharia zilizo thibiti zisio geuka, na ndio kwenye Umoja na asili ya fadhila zote, na mengineyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anakifuta Akitakacho miongoni mwa hukumu na mengineyo, na Anakiacha kisalie Akitakacho miongoni mwa hizo kwa hekima fulani Anayoijua. Na Kwake kuna asili ya Kitabu, nacho ni Al- Lawh Al-Mahfûd,: Ubao uliohifadhiwa ambao zimethibitishwa ndani yake kimaandishi hali za viumbe mpaka Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net