Ar-Ra'd 13:40
الرعدوَإِن مَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ ٱلْبَلَـٰغُ وَعَلَيْنَا ٱلْحِسَابُ
Na ikiwa tutakuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe tu na juu yetu ni hesabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ikiwa tukikuonyesha baadhi ya tuliyo waahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe na juu yetu ni hisabu. [40]
[40] Na tukikuonyesha baadhi ya malipo au adhabu tulizo waahidi, au tukakujaalia ufe kabla ya hayo, ungeli ona kitisho kitacho washukia washirikina, na ungeli ona neema za Waumini! Lakini haya hayakukhusu wewe, juu yako wewe ni kufikisha Ujumbe tu, na kwetu Sisi peke yetu ndio hisabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukikuonesha, ewe Mtume, baadhi ya mateso tuliyowaahidi maadui zako ya udhalili na kuumia ulimwenguni, basi hayo ni yale tuliyowaharakishia. Na tukikufisha kabla hujaona hayo, basi wajibu wako haukuwa isipokuwa ni kutekeleza ulinganizi, na hesabu na malipo ni juu yetu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net