Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 41

Ar-Ra'd 13:41

الرعد

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا نَأْتِى ٱلْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ وَٱللَّهُ يَحْكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكْمِهِۦ ۚ وَهُوَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ

Maana

Je, hawakuona kwamba tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hakuna wa kurekebisha hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhesabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhisabu. [41]

[41] Na hakika dalili za adhabu na kushindwa zipo! Hawaangalii kwamba Sisi tunazifikia nchi walizo kuwa wakizitawala zinachukuliwa na Waumini kidogo kidogo? Na kwa hivyo tunawapunguzia wao ardhi zilio wazunguka. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye wa kuhukumu kushinda na kushindwa, na thawabu na adhabu. Na wala hapana wa kuipinga hukumu yake. Na hisabu yake ni ya mbio mbio, haihitajii kupitiwa na wakati mrefu, kwani Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. Basi ishara zipo! Aya hii ina ukweli ulio fikiliwa na uchunguzi wa kisayansi za hivi sasa, ya kwamba imethibiti kuwa dunia inazunguka, na kuwa inayo mvuto kama simaku. Hayo yamepelekea kubabataa katika ncha mbili za kaskazini na kusini, North Pole na South Pole. Na hivyo ni kupunguka katika ncha mbili za ardhi. Na kadhaalika imejuulikana kuchopoka mbio za sehemu za gasi zilizo funika huu mpira wa dunia kukipindukia nguvu za mvuto wa ardhi, basi hutoka nje ya dunia. Na haya yanatokea mfululizo, na kwa hivyo ardhi, yaani dunia, inakuwa katika hali ya kupunguka moja kwa moja katika ncha zake. Haya yanakuwa kwa kuifasiri ardhi kuwa ni dunia, si nchi ya maadui wa Waumini. Yaelekea taf siri hii kwa Aya hii tukufu, ijapo kuwa wafasiri wengi wamefasiri kuwa muradi wa "ardhi" ni nchi za maadui.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawaoni hawa makafiri kwamba sisi tunaijia ardhi na kuipunguza pembezoni mwake kwa kuwapa Waislamu ushindi wa kuiteka miji ya makafiri na kuishikanisha na miji ya Kiislamu? Na Allah Mtukufu Anaamua, hakuna Mwenye kuurudi uamuzi Wake na hukumu Yake. Na Yeye ni mwepesi wa kuhesabu, basi wasifanye haraka ya kutaka kuletewa adhabu, kwani kila lenye kuja liko karibu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net