Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 42

Ar-Ra'd 13:42

الرعد

وَقَدْ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلِلَّهِ ٱلْمَكْرُ جَمِيعًا ۖ يَعْلَمُ مَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ ۗ وَسَيَعْلَمُ ٱلْكُفَّـٰرُ لِمَنْ عُقْبَى ٱلدَّارِ

Maana

Na walipanga njama wale waliokuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye njama zote. Yeye anajua kile inachochuma kila nafsi. Na makafiri watakuja jua ni ya nani nyumba (njema) ya mwisho (huko Akhera)!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walipanga walio kuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mipango yote. Yeye anajua inayo chuma kila nafsi. Na makafiri watajua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera! [42]

[42] Na walio kuwa kabla yao waliwapangia Mitume wao mipango ya uwovu. Lakini Mwenyezi Mungu Subhanahu ndiye Mwenye mipango yote kwa makafiri walioko sasa na walio watangulia. Na watapata malipo kwa wanayo yatenda, na Yeye anayajua ayatendayo kila kiumbe. Na ikiwa wao hawajui kuwa mwisho mwema ni wa Waumini, basi Siku ya Kiyama watajua kwa kuona nani atapata mwisho mwema kwa kukaa katika Nyumba ya neema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliokuwa kabla yao waliwapangia njama Mitume wao, kama vile hawa walivyokufanyia. Basi vitimbi vyote ni vya Allah Mtukufu, Anatengua vitimbi vyao na kuwarudishia wenyewe wapite patupu na wajute. Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anakijua kile ambacho kila mtu anakichuma, chema au kibaya, na atalipwa kwa hicho. Na watajua makafiri, watakapofika kwa Mola wao, ni nani atakuwa na mwisho mwema baada ya dunia hii. Huo ni wa wafuasi wa Mitume. Katika haya kuna onyo na tishio kwa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net