Ar-Ra'd 13:43
الرعدوَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَسْتَ مُرْسَلًا ۚ قُلْ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۢا بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ وَمَنْ عِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْكِتَـٰبِ
Na wale waliokufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye elimu ya Kitabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya Kitabu. [43]
[43] Na hadi ya ushindani wao hao wanao kanya na hawaikubali Haki ni kukwambia: Ewe Nabii! Wewe si Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu! Basi waambie: Yanitosha mimi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kunihukumia mimi nanyi, na anaye ijua hakika ya Qur'ani na ajabu zake za miujiza ya kushangaza inayo ingia katika akili ziliyo nzima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wenye kumkanusha Nabii wa Allah Mtukufu wanasema, «Ewe Muhammad, hukutumilizwa na Allah Mtukufu.» Waambie, «Inatosha kuwa Allah Mtukufu ni shahidi juu ya ukweli wangu na urongo wenu, na unatosha ushahidi wa wenye ujuzi wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara kati ya wale waliouamini utume wangu na kwamba yale niliokuja nayo yanatoka kwa Allah Mtukufu na akaufuata ukweli na akatoa ushahidi huo waziwazi na asiufiche.»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net