Ar-Ra'd 13:35
الرعدمَّثَلُ ٱلْجَنَّةِ ٱلَّتِى وُعِدَ ٱلْمُتَّقُونَ ۖ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۖ أُكُلُهَا دَآئِمٌ وَظِلُّهَا ۚ تِلْكَ عُقْبَى ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوا۟ ۖ وَّعُقْبَى ٱلْكَـٰفِرِينَ ٱلنَّارُ
Mfano wa Bustani waliyoahidiwa wacha Mungu, kwa chini yake inapita mito, chakula chake ni cha daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliomcha Mungu. Na mwisho wa makafiri ni Moto.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfano wa Bustani waliyo ahidiwa wachamngu, kati yake inapita mito, matunda yake ni ya daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale walio walio jilinda. Na mwisho wa makafiri ni Moto. [35]
[35] Ikiwa hawa watapata adhabu hii, Waumini watapata Pepo na neema zake. Na hayo wamekwisha ahidiwa. Na hali ya Bustani walio ahidiwa wanao simama juu ya Haki na wakaweka kinga baina ya upotovu na Imani, ni kuwa itapitiwa chini ya miti yake maji matamu, na matunda yake ni ya daima hayasiti, na kivuli chake vilevile ni cha daima. Na haya ndiyo malipo ya wale wanao jikinga na shari. Ama makafiri wanao kanya, malipo yao ni kuingia Motoni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sifa ya Pepo ambayo Allah Mtukufu Amewaahidi nayo wale wanaomuogopa na kwamba mito inapita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari, Matunda yake hayamaliziki na kivuli chake hakiondoki. Malipo mema hayo ya Pepo ndio mwisho wa waliomuogopa Allah Mtukufu wakajiepusha na mambo ya kumuasi na wakatekeleza faradhi Zake. Na mwisho wa makafiri ni Moto.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net