Ar-Ra'd 13:34
الرعدلَّهُمْ عَذَابٌ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَشَقُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٍ
Wana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanayo adhabu katika maisha ya dunia, na adhabu ya Akhera hapana shaka ina mashaka zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. [34]
[34] Duniani watapata adhabu kwa kushindwa na kutekwa na kuuliwa, ikiwa Waumini watakwenda katika njia ya Haki. Na hapana shaka adhabu ya Akhera itayo wateremkia ni kali zaidi na ya kudumu zaidi. Hapana wa kuwakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mwenye uwezo wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Makafiri hawa wenye kuzuia njia ya Allah Mtukufu watakuwa na adhabu ngumu katika maisha ya ulimwenguni kwa kuuawa, kutekwa na udhalili. Na kwa hakika, adhabu yao huko Akhera ni nzito zaidi na ni kali zaidi, na hawatakuwa na kizuizi chenye kuwazuia wasipate adhabu ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net