Ar-Ra'd 13:15
الرعدوَلِلَّهِ يَسْجُدُ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَـٰلُهُم بِٱلْغُدُوِّ وَٱلْـَٔاصَالِ ۩
Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi kwa kutii na kwa lazima. Na pia vivuli vyao, asubuhi na jioni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni. [15]
[15] Na vyote viliomo mbinguni na duniani, vitu, watu, majini, na Malaika, vinamnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa matakwa yake na utukufu wake, vikitaka visitake. Hata vivuli vyao kadhaalika, vikirefuka na kufupika kwa mujibu wa nyakati za mchana adhuhuri na jioni, kwa kufuata anavyo amrisha Mwenyezi Mungu na anavyo kataza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Peke Yake wanamsujudia, wakinyenyekea na kufuata, walioko mbinguni na ardhini wote, Waumini wanamsujudia na kumnyenyekea kwa ridhaa na hiari, na makafiri wanamnyenyekea kwa nguvu, kwa kuwa wao wanafanya kiburi kumuabudu na hali yao na maumbile yao yanawakanusha juu ya hilo. Na vivuli vya viumbe vinafuata utukufu wa Allah Mtukufu, vinatembea kulingana na matakwa Yake mwanzo wa mchana na mwisho wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net