Ar-Ra'd 13:14
الرعدلَهُۥ دَعْوَةُ ٱلْحَقِّ ۖ وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَىْءٍ إِلَّا كَبَـٰسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى ٱلْمَآءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَـٰلِغِهِۦ ۚ وَمَا دُعَآءُ ٱلْكَـٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ
Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayakifikii. Na maombi ya makafiri hayako isipokuwa katika upotovu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanao waomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayafiki. Na maombi ya makafiri hayako ila katika upotovu. [14]
[14] Na hayo masanamu wanayo yaomba kwa woga na kutafuta amani badala ya Mwenyezi Mungu pekee hayawajibu wito na maombi yao. Hali yao ni kama mwenye kukunjua kiganja chake akinge maji ya kunywa na kiganja kisifike mdomoni. Na hali yao ikiwa ni hii, basi hizo dua zao haziwi ila kupotea na kukhasirika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni wa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Peke Yake, ulinganizi wa tawḥîd «Hapana mola isipokuwa Allah Mtukufu.» Haabudiwi wala haombwi isipokuwa Yeye. Na waungu ambao wao wanawaabudu badala ya Allah Mtukufu hawaitiki maombi ya mwenye kuwaomba. Na hali yao pamoja na hao waungu ni kama hali ya mwenye kiu anayenyosha vitanga vyake viwili vya mkono kwenye maji kutoka mbali ili yafike kwenye kinywa chake, yakawa hayafiki. Na maombi ya makafiri kwa hao waungu hayakuwa isipokuwa yako mbali na usawa, kwa kuwa wao wanawashirikisha wengine pamoja na Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net