Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 16

Ar-Ra'd 13:16

الرعد

قُلْ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ قُلِ ٱللَّهُ ۚ قُلْ أَفَٱتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِى ٱلظُّلُمَـٰتُ وَٱلنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا۟ لِلَّهِ شُرَكَآءَ خَلَقُوا۟ كَخَلْقِهِۦ فَتَشَـٰبَهَ ٱلْخَلْقُ عَلَيْهِمْ ۚ قُلِ ٱللَّهُ خَـٰلِقُ كُلِّ شَىْءٍ وَهُوَ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّـٰرُ

Maana

Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajimilikii manufaa yoyote wala madhara? Sema: Je, kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au je, huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walioumba kama alivyoumba Yeye, na viumbe hivyo vikawachanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja, Mwenye kushinda!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda! [16]

[16] Mwenyezi Mungu amemuamrisha Nabii wake ajadiliane na washirikina kwa kuwaongoa na kuwabainishia. Akamwambia: Ewe Nabii! Waambie: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi, naye ndiye Mwenye kuzilinda, na Mwenye kuviendesha viliomo humo? Tena uwaeleze jawabu iliyo sawa hiyo wanayo ishindania. Waambie: Huyo ni Mwenyezi Mungu anaye abudiwa kwa haki, hana mwenginewe. Basi ni waajibu wenu mumuabudu Yeye peke yake. Tena waambie: Mnaziona dalili zilizo thibiti zinazo onyesha uumbaji wake kila kitu peke yake? Na juu ya hivyo mnawafanya masanamu kuwa ni miungu, bila ya kukubali kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja! Na haya masanamu hayajifai wenyewe kheri wala shari! Vipi basi mnayafanya sawa na Muumba Mwenye kupanga? Nyinyi mnafanya sawa baina ya Muumba wa kila kitu na asiye miliki kitu! Mmekuwa kama anaye fanya sawa baina ya viwili vinavyo gongana! Basi hebu ni sawa baina ya mwenye kuona na asiye ona? Je, giza totoro na mwangaza unao ng'aa ni sawa? Je, usawa huo unaingia akilini mwao? Au upotovu wao umepita hadi hata wanadai kuwa hayo masanamu yao ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika kuumba na kupanga, hata yakawadanganyikia wasijue mambo ya uumbaji, kama walivyo potea katika kuabudu? Waambie ewe Nabii! Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Muumba wa kila kiliopo. Na Yeye ni peke yake katika kuumba na kuabudiwa, Mwenye kushinda kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie washirikina, ewe Mtume, «Ni nani muumba mbingu na ardhi na mwenye kuziendesha?» Sema, «Allah Mtukufu Ndiye Muuumba Mwenye kuziendesha. Na nyinyi mnalikubali hilo.» Kisha waambie ukiwalazimisha hoja, «Je, mnawafanya wasiokuwa Yeye ni waabudiwa wenu, na hali ya kuwa wao hawawezi kuzinufaisha nafsi zao au kuzidhuru, sembuse kuwanufaisha nyinyi au kuwadhuru, na mkaacha kumuabudu mwenye kuwamiliki wao?» Waambie, «Kwani analingana kwenu nyinyi kafiri, ambaye ni kama kipofu, na Muumini, ambaye ni kama anayeona? Au kwani unalingana kwenu nyinyi ukafiri, ambao ni kama giza, na Imani, ambayo ni kama mwangaza? Au ni kwamba wale wasimamizi wao wanaowafanya ni washirika wa Allah Mtukufu wanaumba kama Anavyoumba, vikawatatiza viumbe vya washirika na viumbe vya Allah Mtukufu, ndipo wakaitakidi kwamba wao wanastahiki kuabudiwa?» Waambie, ewe Mtume, «Allah Mtukufu Aliyetukuka ni Muumba kila kilichoko ambacho hakikuwako; Yeye Ndiye Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake na Yeye Ndiye Aliye mmoja Mwenye kutendesha nguvu Anayestahiki uungu na ibada, na sio masanamu na mizimu isiyodhuru wala kunufaisha».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net