Yusuf 12:33
يوسفقَالَ رَبِّ ٱلسِّجْنُ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا يَدْعُونَنِىٓ إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّى كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ
Yusuf akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Ninapendelea kifungo kuliko haya anayoniitia. Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake hawa, mimi nitaelekea kwao, na nitakuwa katika wajinga.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yusuf akasema: Ee Mola Mlezi wangu! Nastahabu kifungo kuliko haya anayo niitia. Na usipo niondoshea vitimbi vya wanawake mimi nitamili kwao, na nitakuwa katika wajinga. [33]
[33] Yusuf akasema naye alisikia vile vitishio, na akasikia kwa wale wanawake nasiha ya kuwa amkubalie, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nakhiari kifungo kuliko hayo anayo nitakia huyu mwanamke. Kwani hayo ni kukuasi Wewe. Na kama Wewe hunikingi na shari ya vitimbi vyao na hila zao nitakuja wakubalia, na nitakuwa miongoni mwa wajinga walio potea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yûsuf akasema, akijilinda na shari zao na vitimbi vyao, «Ewe Mola wangu! Jela ni bora kwangu kuliko yale wanayoniitia ya kufanya machafu. Na usiponiepushia vitimbi vyao, nitalemea kwao na nitakuwa ni miongoni mwa wachache wa akili wenye kujifanyia madhambi kwa ujinga wao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net