Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yusuf
Sura ya 12

Yusuf

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 33

قَالَ رَبِّ ٱلسِّجْنُ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا يَدْعُونَنِىٓ إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّى كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ 33

33. Hapo, Yusuf akashikamana na Mola wake Mlezi, na akamwomba msaada katika vitimbi vyao hivi. Na "akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Ninapendelea kifungo kuliko haya anayoniitia." Na haya yanaashiria kuwa wale wanawake walianza kumtia moyo Yusuf kwamba amtii bibi yake, na wakaanza kumfanyia njama katika hilo, lakini akapendelea jela na adhabu ya kiduniani kuliko starehe za sasa zenye kusababisha adhabu kubwa. "Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake, mimi nitaelekea kwao." Yaani, nitaelekea kwao. Kwa maana, mimi ni dhaifu na mnyonge usiponilinda na ubaya huu, nitaelekea kwao. "Na nitakuwa katika wajinga" kwa maana huu ni ujinga, kwa kuwa ni kupendelea starehe ndogo ihuzunishayo kuliko starehe za mfululizo na matamanio mbalimbali katika Bustani za neema. Na anayependelea haya kuliko yale, basi ni nani mjinga zaidi yake? Kwa maana, elimu na akili vinaitia kutanguliza masilahi makubwa zaidi kati ya mawili hayo na starehe kubwa zaidi kati ya starehe mbili hizo, na hupendelea kile chenye mwisho wa kusifiwa.