Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 32

Yusuf 12:32

يوسف

قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِى لُمْتُنَّنِى فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفْسِهِۦ فَٱسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ ٱلصَّـٰغِرِينَ

Maana

Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliyenilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na asipofanya ninayomwamrisha, basi hakuna shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio duni kabisa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliye nilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na akitofanya ninayo muamrisha basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio chini kabisa. [32]

[32] Tena mke wa Mheshimiwa alisema kufuatiliza maneno yao: Huyu kijana ambaye uzuri wake umekuzugeni na ukakuemeeni hata yakatokea yaliyo tokea ndiye ambaye nyinyi mliye nilaumu kwa ajili yake! Na mimi kweli nilimtaka, na nikafanya juhudi kumghuri anikubalie, naye akajizuia na akakataa. Kama kwamba vile anavyo kataa ndio anazidi kumtia hamu yule mwanamke! Akasema mwanamke: Na mimi naapa! Kama hafanyi ninayo muamrisha atapata adhabu ya kifungo, na atakuwa katika madhalili wenye kudharauliwa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mke wa kiongozi akasema kuwaambia wanawake waliojikata mikono yao, «Haya ndiyo yaliyowapata kwa kumuona yeye. Aliyefanya mpatikane na haya ni huyu kijana ambaye nyinyi mumenilaumu kusalitika naye. Kwa kweli nilimtaka na nikajaribu kumvutia ili anikubalie, akajizuia na akakataa. Na asipofanya ninachomuamuru mbeleni, atateswa kwa kutiwa jela na hapo atakuwa ni miongoni mwa wanyonge.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net