Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 31

Yusuf 12:31

يوسف

فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَـًٔا وَءَاتَتْ كُلَّ وَٰحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ ٱخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُۥٓ أَكْبَرْنَهُۥ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَـٰشَ لِلَّهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ

Maana

Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita, na akawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: "Jitokeze mbele yao." Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikatakata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alipo sikia yule bibi masengenyo yao aliwaita, na akawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: Tokeza mbele yao. Basi walipo mwona waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi! Huyu si mwanaadamu. Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu. [31]

[31] Yule bibi alipo yasikia masengenyo yao wale wanawake na kuwa wanamsema kwa vibaya, aliwaalika nyumbani kwake na akawapangia matakia na mito ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu, baada ya kwisha hudhuria na wakakaa wakiegemea. Akawaletea chakula na visu vya kulia. Akamwambia Yusuf: Hebu watokee! Alipotokeza wakamwona walistaajabu. Uzuri wake ulio pita mpaka uliwatwaa wasijitambue, wakawa wanajikata mikono yao jinsi ya kushtuka kwao, na huku wanadhani wanakata chakula! Wakasema kwa mastaajabu na kushituka: Hasha Lillahi! Mungu apishe mbali! Huyu tunaye mwona si binaadamu! Hapana binaadamu mwenye uzuri namna hii, na mwenye jamali kama hivi, na usafi kama huu, na kunyooka kama huku! Huyu ni Malaika tu, mwenye uzuri huu, na sifa hizi zilio timia!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Aliposikia mke wa Kiongozi kusengenya kwao na hila zao za kumtukana yeye, aliwatumia ujumbe na kuwaita kuja kumtembelea, na akatayarisha mito ya kutegemea na chakula cha kula, na akampa kila mmoja miongoni mwao kisu cha kukatia chakula kisha akasema kumwambia Yûsuf, «Jitokeze kwao.» Walipomshuhudia, walimuona ni kitu kikubwa chenye haiba, na wakashikwa na babaiko la uzuri wake na kuvutia kwake, wakajikata mikono yao katika hali ya kukata chakula kwa babaiko kuu na mshangao, na wakasema kwa kustaajabu, «Twajilinda na Allah Mtukufu! Huyu si binadamu!» kwa kuwa uzuri wake sio ule ujulikanao kwa wanadamu, «Huyu si mwingine isipokuwa ni mtukufu miongoni mwa Malaika».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net