Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 30

Yusuf 12:30

يوسف

وَقَالَ نِسْوَةٌ فِى ٱلْمَدِينَةِ ٱمْرَأَتُ ٱلْعَزِيزِ تُرَٰوِدُ فَتَىٰهَا عَن نَّفْسِهِۦ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَىٰهَا فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake bila ya yeye kumtaka! Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni. Sisi hakika tunamwona yuko katika upotovu ulio dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake ! Hakika amesalitika kwa mapenzi. Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio dhaahiri. [30]

[30] Khabari zikawafikia baadhi ya wanawake wa mjini, wakazungumza wakisema: Mke wa Mheshimiwa anamzaini mtumishi wake na anamkhadaa amkubalie anayo yataka kwake! Ama kweli amesalitika kwa mahaba hata hajitambui! Hakika sisi tunaamini kuwa kwa mwendo wake huu ameingia kwenye upotovu na makosa yaliyo wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Habari ziliwafikia wanawake mjini wakaizungumza kuhusu hizo na wakasema kwa njia ya kumpinga mke wa kiongozi, «Mke wa Bwana anajaribu kumtaka mtumwa wake na amwita amjie. Na mapenzi yake yamefikia kwenye ngozi ya moyo wake. Hakika sisi tunamuona yeye kuwa yuko kwenye upotevu waziwazi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net