Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 29

Yusuf 12:29

يوسف

يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۚ وَٱسْتَغْفِرِى لِذَنۢبِكِ ۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ ٱلْخَاطِـِٔينَ

Maana

Yusuf! Achilia mbali haya. Na wewe mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Hakika wewe ni katika waliofanya makosa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yusuf! Wachilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Kwa hakika wewe ni katika walio fanya makosa. [29]

[29] Ewe Yusuf wachilia mbali mambo haya, na wewe yafiche wala usiyaseme. Na wewe, mwanamke, omba maghfira kwa dhambi yako. Hapana shaka kuwa wewe ni katika wenye dhambi, wenye kuyakusudia makosa, na kutenda maasi, na kuwasingizia wengine uasi wasio ufanya!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Akasema kiongozi wa Misri, «Ewe Yûsuf! acha kutaja mambo yaliyokuwa kutoka kwake na usimwambie yoyote. Na uombe msamaha wa dhambi zako kwa Mola wako, ewe mwanamke, iwapo wewe ni miongoni mwa wale waliofanya hatia kwa kumtaka Yûsuf kimapenzi bila ya yeye kutaka na kwa kumzulia urongo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net