Yusuf 12:28
يوسففَلَمَّا رَءَا قَمِيصَهُۥ قُدَّ مِن دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُۥ مِن كَيْدِكُنَّ ۖ إِنَّ كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ
Basi yule bwana alipoona shati lake limechanwa kwa nyuma, akasema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Bila ya shaka vitimbi vyenu ni vikuu. [28]
[28] Mume alipoona kuwa kanzu ya Yusuf imechanwa mgongoni alimwambia mkewe: Huku kumtuhumu kwako kijana kwa yaliyo tokea na hali yeye hana makosa, ni katika vitimbi vyenu, enyi wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu mno!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yule mume alipoiona nguo ya Yûsuf imeraruliwa kwa nyuma alijua kwamba Yûsuf hana hatia na akasema kumwambia mke wake, «Urongo huu uliomtuhumu nao kijana huyu ni katika jumla ya vitimbi vyenu, enyi wanawake, kwani vitimbi vyenu ni vikubwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net