Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 34

Yusuf 12:34

يوسف

فَٱسْتَجَابَ لَهُۥ رَبُّهُۥ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye ni Msikizi Mjuzi. [34]

[34] Mwenyezi Mungu akamuitikia, na akamuepusha na shari ya vitimbi vyao. Hakika Yeye peke yake ndiye Mwenye kusikia maombi ya wenye kukimbilia kwake, na Mwenye kujua yanao wafaa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Akamkubalia Yûsuf maombi yake, akamwepushia kile alichotaka mke wa Kiongozi na marafiki zake kutoka kwake cha kumuasi Allah Mtukufu. Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuyasikia maombi ya Yûsuf na maombi ya kila mwenye kuomba kati ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyajua matakwa yake, haja zake na kile kinachomfaa, na pia haja za viumbe Vyake vyote na yale yanayowafaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net