Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 35

Yusuf 12:35

يوسف

ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّنۢ بَعْدِ مَا رَأَوُا۟ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَيَسْجُنُنَّهُۥ حَتَّىٰ حِينٍ

Maana

Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara mbalimbali kuwa lazima wamfunge kwa muda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara kuwa wamfunge kwa muda. [35]

[35] Kisha ikadhihiri rai ya Mheshimiwa na watu wake, baada ya kwisha ona dalili zilizo wazi kuwa Yusuf hana makosa. Wakakubaliana rai hii, na wakaapa kuitimiza. Nayo ni kumtia yeye gerezani kwa muda mfupi au mrefu, ili kumkinga mkewe na maneno mabaya, na kumuepusha na masengenyo ya watu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha ikamdhihirikia waziri na marafiki zake, baada ya kuziona dalili za kuwa Yûsuf hana hatia na amejiepusha na machafu, wamfunge mpaka muda fulani, mrefu au mfupi, ili kuzuia fedheha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net