Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 36

Yusuf 12:36

يوسف

وَدَخَلَ مَعَهُ ٱلسِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَآ إِنِّىٓ أَرَىٰنِىٓ أَعْصِرُ خَمْرًا ۖ وَقَالَ ٱلْـَٔاخَرُ إِنِّىٓ أَرَىٰنِىٓ أَحْمِلُ فَوْقَ رَأْسِى خُبْزًا تَأْكُلُ ٱلطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِۦٓ ۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Na wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota kuwa ninakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Hakika mimi nimeota kuwa nimebeba mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanakula kwayo. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota nakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Mimi nimeota nimebeba mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanaila. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wema. [36]

[36] Wakaingia pamoja na Yusuf vijana wawili katika watumishi wa Mfalme. Mmoja wao akasema: Mimi nimeota usingizini kuwa ninakamua zabibu kutengeneza mvinyo. Mwingine akasema: Mimi nimeota nimebeba kichwani mwangu mikate, na ndege wanaila! Hebu tuambie, ewe Yusuf, tafsiri ya haya tuliyo ota, na mambo yetu yataishia vipi. Sisi tunaamini kuwa wewe ni katika watu wanao sifika kwa wema na kujua tafsiri za ndoto.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakaingia jela pamoja na yeye vijana wawili. Mmoja wao akasema, «Mimi nimeota usingizini kwamba mimi nakamua zabibu ili ziwe pombe.» Na mwingine alisema, «Mimi nimeota kwamba nabeba mkate juu ya kichwa changu na ndege wanaula. Wakasema, «Tupe habari, ewe Yûsuf, ya tafsiri za ndoto tulizoziota. Sisi tunakuona wewe ni miongoni mwa wale wanaofanya wema katika kuabudu kwao Allah Mtukufu na kuingiliana kwao na viumbe Wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net