Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 37

Yusuf 12:37

يوسف

قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِۦٓ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِۦ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِى رَبِّىٓ ۚ إِنِّى تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ كَـٰفِرُونَ

Maana

Akasema: Hakitawajia chakula mtakachoruzukiwa isipokuwa nitawaambia hakika yake kabla ya kuwajia. Hayo ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya kaumu wasiomuamini Mwenyezi Mungu, na wakawa wameikufuru Akhera.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Hakitakufikilieni chakula mtakacho pewa ila nitakwambieni hakika yake kabla hakijakufikieni. Haya ni katika yale aliyo nifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasio muamini Mwenyezi Mungu, na wakawa hawaiamini Akhera. [37]

[37] Yusuf akawaambia kutilia mkazo yale waliyo yajua kwake Yusuf: Hakitowahi kukufikieni chakula kuwa ni riziki mliyo kadiriwa ila nami nitakwambieni kitavyo kujieni kabla ya kukufikieni. Na nitakutajieni mapishi yake na vipi kilivyo. Namna hivyo ndivyo tafsiri ya ndoto na khabari zilizo fichikana katika alivyo nifunza Mola wangu Mlezi na akanifunulia, kwani nilimtakasia Yeye tu ibada yangu. Na nikakataa kumshirikisha na kitu chochote. Na nikajitenga mbali na dini ya watu wasio msadiki Mwenyezi Mungu, na wala hawamuamini Yeye kwa njia iliyo sawa, nao wanaikanya Akhera na hisabu zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yûsuf aliwaambia, «Hamtajiwa na riziki ya chakula kwa namna yoyote ile, isipokuwa mimi nitawapa tafsiri yake kabla ya kuwajia. Tafsiri hiyo nitakayowapa nyinyi wawili ni miongoni mwa yale niliyofundishwa na Mola wangu. Mimi nimemuamini na nimemtakasia ibada na nimejiepusha na dini ya wasiomuamini Allah Mtukufu wala kuamini kufufuliwa na kuhesabiwa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net