Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 38

Yusuf 12:38

يوسف

وَٱتَّبَعْتُ مِلَّةَ ءَابَآءِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشْرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَىْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ عَلَيْنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ

Maana

Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Haikutufailia sisi kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Hatuna haki ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu; lakini watu wengi hawashukuru. [38]

[38] Mimi nimeacha mila ya hawa makafiri, na nikafuata Dini ya baba zangu Ibrahim, na Is-haaq, na Yaa'qub. Nikamuabudu Mwenyezi Mungu pekee. Haitufalii sisi kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika yeyote yule, akiwa Malaika, au jini, au mwanaadamu, licha ya masanamu ambayo hayaleti manufaa wala madhara, wala hayasikii, wala hayaoni! Hiyo ndiyo Tawhidi aliyo tutunukia Mwenyezi Mungu sisi na watu wote, kwa vile alivyo tuamrisha tuwafikilishie ujumbe. Lakini wengi wa watu hawaipokei fadhila hii kwa shukrani, bali wanaikataa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Na nimefuata Dini ya baba zangu: Ibrãhîm, Is’hãq na Ya‛qûb, ndipo nikaamuabudu Allah Mtukufu Peke Yake. Haikuwa kwetu sisi kumfanyia Allah Mtukufu mshirika katika kumuabudu. Kumpwekesha Allah Mtukufu huko, kwa kumhusu Yeye Peke Yake kwa ibada, ni miongoni mwa yale ambayo Allah Mtukufu Ametutunukia sisi na watu, lakini wengi zaidi wa watu hawamshukuru Allah Mtukufu kwa neema ya upwekeshaji wa Allah Mtukufu na Imani».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net