Yusuf 12:10
يوسفقَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا۟ يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِى غَيَـٰبَتِ ٱلْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ ٱلسَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَـٰعِلِينَ
Akasema msemaji miongoni mwao: Msimuue Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima. Baadhi ya wasafiri watakuja mwokota; ikiwa kweli mnataka kufanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema msemaji kati yao: Msimuuwe Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima. Wasafiri watakuja mwokota; kama nyinyi mna sharti ya kufanya jambo. [10]
[10] Mmoja wao katika wasemaji alisema: Msimuuwe Yusuf. Hayo ni makosa makubwa. Lakini mtupeni asipo onekana ndani ya kisima, baadhi ya wapita njia watakuja mwokota, watapo tumbukiza ndoo yao kisimani. Hao watakwenda naye pahala pambali nanyi na baba yenu vile vile. Haya ikiwa nyinyi mna lazima mumpeleke mbali na mtimize kwa kitendo hayo mtakayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema mwenye kusema, miongoni mwa ndugu za Yûsuf, «Msimuue Yûsuf, na mtupeni ndani ya kisima ataokotwa na wapita njia miongoni mwa wasafiri, na hapo mtapumzika na yeye; na hakuna haja ya nyinyi kumuua, iwapo muna azma ya kulifanya hilo mnalolisema».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net