Yusuf 12:9
يوسفٱقْتُلُوا۟ يُوسُفَ أَوِ ٱطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا۟ مِنۢ بَعْدِهِۦ قَوْمًا صَـٰلِحِينَ
Muueni Yusuf, au mtupeni nchi ya mbali ili uso wa baba yenu uwaelekee nyinyi tu. Na baada ya haya mtakuwa kaumu njema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya mtakuwa watu wema. [9]
[9] Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi iliyo mbali na baba yenu, asiyo weza kuifikia. Yatakuwafikieni nyinyi tu mapenzi ya baba yenu, na atakuelekeeni nyinyi tu. Na baada ya kumtenga Yusuf naye kwa kumuuwa au kumhamisha mtakuwa watu wema. Kwani Mwenyezi Mungu atakubali toba yenu, na baba yenu atapokea udhuru wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Muueni Yûsuf! Au mtupeni kwenye ardhi isiyojulikana iliyo mbali na mji, hapo yatasafika kwenu mapenzi ya baba yenu na muelekeo wake kwenu, na hatageuka kwa wengine na kuacha kushughulika na nyinyi, na mtakuwa, baada ya kumuua Yûsuf au kumpoteza, ni wenye kutubia kwa Allah Mtukufu na kumuomba msamaha baada ya kosa lenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net