Yusuf 12:8
يوسفإِذْ قَالُوا۟ لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰٓ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
Pale waliposema: Hakika Yusuf na kakaye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, ilhali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yuko katika upotovu wa dhahiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Pale walipo sema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, hali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa dhaahiri. [8]
[8] Walipo semezana nduguze Yusuf kwa baba: Bila ya shaka Yusuf na nduguye kwa baba na mama wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi. Na sisi ni kikundi chenye nguvu, chenye kumfaa yeye zaidi kuliko wao! Hakika baba yetu kwa kumfadhilisha Yusuf na nduguye kuliko sisi yumo makosani, na yuko mbali na haki. Yalio sawa yapo wazi yanaonekana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waliposema ndugu zake Yûsuf wa kwa baba kuambiana wao kwa wao, Hakika Yûsuf na ndugu yake wa kwa baba na mama wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi. Anawafanya wao bora juu yetu, na sisi ni kundi lenye idadi kubwa. Hakika baba yetu yuko makosani waziwazi, kwa kuwa amewafanya wao ni bora juu yetu bila ya sababu tunayoiyona yenye kupelekea kufanya hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net