Yusuf 12:7
يوسفلَّقَدْ كَانَ فِى يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِۦٓ ءَايَـٰتٌ لِّلسَّآئِلِينَ
Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanaouliza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanao uliza. [7]
[7] Hakika katika kisa cha Yusuf na nduguze zipo dalili na mazingatio kwa waulizao, wenye kutaka kujua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika katika kisa cha Yûsuf na ndugu zake kuna mazingatio na dalili za uwezo wa Allah Mtukufu na hekima Yake kwa anayeuliza habari zao na akataka kuzijua.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net